Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Pet 5:6
Kukumbuka yale yote Mungu ametenda.
Siku 5
Ni tabia yetu ya asili kutazamia siku zijazo lakini tusisahau kamwe siku zilizopita. Mpango huu umechapishwa kwa ajili yako katika siku 5 zijazo kukukumbusha yote ambayo Mungu amekutendea katika kukutengeneza kuwa ulivyo leo Kila siku utapata somo la biblia na ibada fupi iliyoundwa kukusaidia kukumbuka matukio muhimu katika kutembea kwako na Kristo.
Ninakungoja Hapa, Njia ya Majirio ya Tumaini
Siku 7
Majirio ni majira ya matarajio na maandalizi. Ungana na mchungaji na mwandishi Louie Giglo katika safari ya majirio kupata ufahamu ya kuwa kungojea siyo kuharibu hasa unapomngojea Bwana. Shikilia nafasi ya kupata ufunuo na tumaini katika safari hii ya majirio. Katika siku saba zijazo utapata amani na himizo kwa nafsi yako kama vile matarajio kuelekea sherehe!
Yesu Ananipenda
Siku 7
Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu.