Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Yoh 1:8
Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya Asubuhi
Siku 4
Dk. Tony Evans anatoa maombi ya jina la Yesu, nyota ya asubuhi. Sala ya kuabudu, maungamo, shukrani na dua kumhusu Nyota ya asubuhi, Yule anayeangazia njia yetu.
Vitendo vya Toba
Siku 5
Toba ni moja ya hatua muhimu sote huchukua tunapokuja kumjua Yesu kristo kama mwongozi wa maisha yetu. Toba ni kitendo chetu na msamaha ni majibu ya Mungu kwetu kutokana na mapenzi yake kamili kwa ajili yetu. Ndani ya siku tano na kupitia masomo haya, utapokea somo la biblia kila siku na ibada fupi iliyoundwa kukusaidia kuelewa vyema umuhimu wa toba katika kutembea kwetu na Kristo.
Adui wa Moyo
Siku 5
Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adui wanne wa moyo — hatia, hasira, tamaa, na wivu — na kukufunza jinsi ya kuwaondoa.
Naweza Kweli Kushinda Dhambi na Majaribu?
Siku 5
Umewahi kujiuliza, “Mbona bado napambana na dhambi hiyo?” Hata mtume Paulo alisema hivyo katika Warumi 7:15: “ Sifanyi ninachotaka, lakini nafanya kile ninachochukia.” Je, tunazuiaje dhambi kusimamisha maisha yetu ya kiroho? Je, hata inawezekana? Hebu tujadili dhambi, majaribu, Shetani, na, kwa shukrani, upendo wa Mungu.