1
Mwanzo 9:12-13
BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA
Tena Mungu akasema, “Hii ndiyo alama ya agano ninalofanya kati yangu nanyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi kwa vizazi vyote vijavyo. Naweka upinde wangu mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano kati yangu na dunia.
Krahaso
Eksploroni Mwanzo 9:12-13
2
Mwanzo 9:16
Huo upinde utakapotokea mawinguni, nitauona na kulikumbuka agano hilo la milele kati yangu na viumbe vyote hai duniani.”
Eksploroni Mwanzo 9:16
3
Mwanzo 9:6
Amwagaye damu ya binadamu, damu yake itamwagwa na binadamu; maana binadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu.
Eksploroni Mwanzo 9:6
4
Mwanzo 9:1
Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni, muongezeke, mkaijaze nchi.
Eksploroni Mwanzo 9:1
5
Mwanzo 9:3
Wanyama wote hai watakuwa chakula chenu kama vile nilivyowapa mimea kuwa chakula chenu.
Eksploroni Mwanzo 9:3
6
Mwanzo 9:2
Wanyama wote, ndege wote wa angani, viumbe wote watambaao juu ya nchi na samaki wote wa baharini watakuwa na hofu na kuwaogopa nyinyi. Wote wamewekwa chini ya mamlaka yenu.
Eksploroni Mwanzo 9:2
7
Mwanzo 9:7
Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni kwa wingi, mkaongezeke nchini.”
Eksploroni Mwanzo 9:7
Kreu
Bibla
Plane
Video