Mattayo MT. 24:37-39
Mattayo MT. 24:37-39 SWZZB1921
Lakini kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa maana kama vile siku ziie zilizokuwa kabla ya gharika watu walivyokuwa wakila, wakinywa, wakioa, wakioza, hatta siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hatta gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo na kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.