Mattayo MT. 17:17-18
Mattayo MT. 17:17-18 SWZZB1921
Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini na kipotofu, nitakuwa pamoja nanyi hatta lini? Nitachukuliana nanyi hatta lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkaripia pepo, akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.