1
Yohana MT. 5:24
New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921
Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.
Bera saman
Njòttu Yohana MT. 5:24
2
Yohana MT. 5:6
Yesu alipomwona huyu amelala, akijua ya kuwa amekuwa hali hii siku nyingi, akamwambia, Wataka kuwa nizima?
Njòttu Yohana MT. 5:6
3
Yohana MT. 5:39-40
Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia: wala hamtaki kuja kwangu, mpate kuwa na uzima.
Njòttu Yohana MT. 5:39-40
4
Yohana MT. 5:8-9
Yesu akamwambia, Simama, jitwike kitanda chako, ukaende. Marra yule mtu akawa mzima, akajitwika kitanda chake, akaenda. Bassi ilikuwa sabato siku ile.
Njòttu Yohana MT. 5:8-9
5
Yohana MT. 5:19
Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile.
Njòttu Yohana MT. 5:19
Heim
Biblía
Áætlanir
Myndbönd