1
Mwanzo 12:2-3
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu 2024
“Nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, Nitalikuza jina lako, nawe utakuwa baraka. Nitawabariki wale wanaokubariki, na yeyote akulaaniye nitamlaani; na kupitia kwako mataifa yote duniani yatabarikiwa.”
Konpare
Eksplore Mwanzo 12:2-3
2
Mwanzo 12:1
Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonesha.
Eksplore Mwanzo 12:1
3
Mwanzo 12:4
Hivyo Abramu akaondoka kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwambia; naye Lutu akaondoka pamoja naye. Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na umri wa miaka sabini na tano.
Eksplore Mwanzo 12:4
4
Mwanzo 12:7
Mwenyezi Mungu akamtokea Abramu, akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapo akamjengea madhabahu Mwenyezi Mungu aliyekuwa amemtokea.
Eksplore Mwanzo 12:7
Akèy
Bib
Plan yo
Videyo