1
Yohana 10:10
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Mwizi huja ili aibe, aue na aangamize. Mimi nimekuja ili wapate uzima, kisha wawe nao tele.
Konpare
Eksplore Yohana 10:10
2
Yohana 10:11
“Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
Eksplore Yohana 10:11
3
Yohana 10:27
Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata.
Eksplore Yohana 10:27
4
Yohana 10:28
Nami ninawapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu.
Eksplore Yohana 10:28
5
Yohana 10:9
Mimi ndimi lango. Yeyote anayeingia zizini kupitia kwangu ataokoka. Ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
Eksplore Yohana 10:9
6
Yohana 10:14
“Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu, nao kondoo wangu wananijua.
Eksplore Yohana 10:14
7
Yohana 10:29-30
Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote, na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake. Mimi na Baba yangu tu umoja.”
Eksplore Yohana 10:29-30
8
Yohana 10:15
Kama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, ndivyo nami ninautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
Eksplore Yohana 10:15
9
Yohana 10:18
Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu, na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”
Eksplore Yohana 10:18
10
Yohana 10:7
Kwa hiyo Isa akasema nao tena, akawaambia, “Amin, amin nawaambia, mimi ndimi lango la kondoo.
Eksplore Yohana 10:7
11
Yohana 10:12
Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Anapomwona mbwa-mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa-mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya.
Eksplore Yohana 10:12
12
Yohana 10:1
“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang’anyi.
Eksplore Yohana 10:1
Akèy
Bib
Plan yo
Videyo