1
Mathayo 4:4
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
TKU
Yesu akajibu, “Maandiko yanasema, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Mungu.’”
Compare
Avasta Mathayo 4:4
2
Mathayo 4:10
Yesu akamjibu Shetani akamwambia, “Ondoka kwangu Shetani! Kwani Maandiko yanasema, ‘Umwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake!’”
Avasta Mathayo 4:10
3
Mathayo 4:7
Yesu akamjibu, “Pia, Maandiko yanasema, ‘usimjaribu Bwana Mungu wako.’”
Avasta Mathayo 4:7
4
Mathayo 4:1-2
Kisha Roho Mtakatifu akamwongoza Yesu hadi nyikani ili akajaribiwe na Shetani. Baada ya Yesu kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, akaumwa njaa sana.
Avasta Mathayo 4:1-2
5
Mathayo 4:19-20
Yesu akawaambia, “Njooni, mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa aina nyingine. Nitawafundisha jinsi ya kukusanya watu badala ya samaki.” Mara moja, Simoni na Andrea wakaziacha nyavu zao na kumfuata Yesu papo hapo.
Avasta Mathayo 4:19-20
6
Mathayo 4:17
Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia watu ujumbe wake unaosema, “Mbadili mioyo yenu na maisha yenu pia, kwa sababu Ufalme wa Mungu umewafikia.”
Avasta Mathayo 4:17
Home
Bible
Plans
Videod