YouVersion Logo
Search Icon

Ezr 10

10
Watu Wamjibu Ezra
1 # Dan 9:20; 2 Nya 20:9 Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, wakamkusanyikia katika Israeli wote kusanyiko kubwa sana la wanaume, na wanawake, na watoto; maana watu hao walikuwa wakilia sana. 2#Kut 34:13Hata Shekania, mwana wa Yehieli, mmoja wa wana wa Elamu, akajibu, akamwambia Ezra, Sisi tumemkosa Mungu wetu, nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi; lakini kungaliko tumaini kwa Israeli katika jambo hili. 3#Ezr 9:4; Zab 119:53,120; Isa 66:2; Kum 7:2,3Haya basi! Na tufanye agano na Mungu wetu, kuachana na wake zetu, na wale waliozaliwa nao, tukilifuata shauri la bwana wangu, na shauri la hao wanaoitetemekea amri ya Mungu wetu; mambo haya na yatendeke kwa kuifuata torati. 4#1 Nya 28:10; Isa 35:3,4Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende. 5#Neh 5:12Ndipo Ezra akaondoka, akawaapisha wakuu wa makuhani, na Walawi, na Israeli wote, ya kwamba watafanya kama hayo. Basi wakaapa.
Wake wa Ndoa za Mseto na Watoto wao Wafukuzwa
6 # Kum 9:18 Kisha Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu, akaingia katika chumba cha Yehohanani, mwana wa Eliashibu; hata, alipofika huko, hakula mkate, wala hakunywa maji; kwa maana alilia kwa sababu ya kosa lile la watu wa uhamisho. 7Wakapiga mbiu katika Yuda yote na Yerusalemu, ya kwamba wana wote wa uhamisho wakusanyike pamoja huko Yerusalemu; 8#Law 27:28; Yos 6:19na ya kwamba mtu awaye yote asiyekuja katika muda wa siku tatu, kwa shauri lile la wakuu na wazee, basi aondolewe mali zake zote, akatengwe yeye mwenyewe na mkutano wa uhamisho.
9 # 1 Sam 12:18 Ndipo wanaume wote wa Yuda na Benyamini wakakusanyika katika muda wa siku tatu; ulikuwa mwezi wa kenda, siku ya ishirini ya mwezi; na watu wote wakaketi katika uwanja mbele ya nyumba ya Mungu, wakitetemeka kwa sababu ya neno hilo, na kwa sababu ya mvua kubwa. 10Kisha Ezra, kuhani, akasimama, akawaambia, Mmekosa, mmeoa wanawake wageni, kuiongeza hatia ya Israeli. 11#Mit 28:13; Yer 3:13; Isa 1:16,17; Rum 12:2Sasa basi, ungameni mbele za BWANA, Mungu wa baba zenu, mkatende alipendalo; mkajitenge na watu wa nchi, tena na wanawake wageni. 12Ndipo mkutano wote wakajibu, wakasema, kwa sauti kuu, Kama ulivyosema katika habari yetu, ndivyo vitupasavyo kutenda. 13Lakini watu hawa ni wengi, tena ni wakati wa mvua nyingi, nasi hatuwezi kusimama nje, tena kazi hii si kazi ya siku moja, wala ya siku mbili; maana tumekosa sana katika jambo hili. 14#Hes 25:4; 2 Fal 23:26; 2 Nya 28:11-13; 29:10; 30:8; Zab 78:38; Isa 12:1Basi maakida wetu na wawekwe kwa ajili ya mkutano wote, na watu wote walio katika miji yetu, waliooa wanawake wageni, na waje nyakati zilizoamriwa, tena pamoja nao na waje wazee wa kila mji, na makadhi wa miji hiyo, hata ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapotuondokea mbali, jambo hili likamalizike. 15Yonathani, mwana wa Asaheli, na Yazeya, mwana wa Tikwa, hawa peke yao ndio waliosimama kulipinga neno hilo; na Meshulamu, na Shabethai Mlawi, wakawasaidia. 16Basi wana wa uhamisho wakafanya hivyo. Na Ezra, kuhani, akatengwa, pamoja na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa, kwa hesabu ya mbari ya baba zao; na hao wote kwa majina yao. Wakaketi siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, ili kulichunguza jambo hilo. 17Wakamaliza mambo ya wanaume wote, waliokuwa wameoa wanawake wageni, siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza.
18 # Ezr 5:2; Hag 1:1,12; Zek 3:1; 6:11 Basi, miongoni mwa makuhani walionekana wengine waliokuwa wameoa wanawake wageni; wa wana wa Yoshua, mwana wa Yosadaki, na nduguze; Maaseya, na Eliezeri, na Yaribu, na Gedalia. 19#2 Fal 10:15; 1 Nya 29:24; 2 Nya 30:8; Gal 2:9; Mit 6:1; 22:26; Law 5:15; 6:4-6Nao wakatoa ahadi ya kwamba wataachana na wake zao; na kwa kuwa walikuwa na hatia, wakatoa kondoo mume kwa hatia yao. 20Na wa wana wa Imeri; Hanani, na Zebadia. 21Na wa wana wa Harimu; Maaseya, na Eliya, na Shemaya, na Yehieli, na Uzia. 22Na wa wana wa Pashuri; Elioenai, na Maaseya, na Ishmaeli, na Nethaneli, na Yozabadi, na Elasa. 23Na wa Walawi; Yozabadi, na Shimei, na Kelaya (ndiye Kelita), na Pethahia, na Yuda, na Eliezeri. 24Na wa waimbaji; Eliashibu. Na wa mabawabu; Shalumu, na Telemu, na Uri.
25 # Ezr 2:3; 8:3; Neh 7:8 Na wa Israeli; wa wana wa Paroshi; Ramia, na Izia, na Malkiya, na Miyamini, na Eleazari, na Malkiya, na Benaya. 26Na wa wana wa Elamu; Matania, na Zekaria, na Yehieli, na Abdi, na Yeremothi, na Eliya. 27#Ezr 2:8; Neh 7:13Na wa wana wa Zatu; Elioenai, na Eliashibu, na Matania, na Yeremothi, na Zabadi, na Aziza. 28Na wa wana wa Bebai; Yehohanani, na Hanania, na Zakai, na Athlai. 29Na wa wana wa Bani; Meshulamu, na Maluki, na Adaya, na Yashubu, na Sheali, na Yeremothi. 30Na wa wana wa Pahath-Moabu; Adna, na Kelali, na Benaya, na Maaseya, na Matania, na Besaleli, na Binui, na Manase. 31#Neh 3:11Na wa wana wa Harimu; Eliezeri, na Ishiya, na Malkiya, na Shemaya, na Shimeoni, 32na Benyamini, na Maluki, na Shemaria. 33Na wa wana wa Hashumu; Matenai, na Matata, na Zabadi, na Elifeleti, na Yeremai, na Manase, na Shimei. 34Na wa wana wa Bani; Maadai, na Amramu, na Ueli, 35na Benaya, na Bedeya, na Keluhi, 36na Wania, na Meremothi, na Eliashibu, 37na Matania, na Matenai, na Yaasu. 38Na wa wana wa Binui; Shimei, 39na Shelemia, na Nathani, na Adaya, 40na Maknadebai, na Shashai, na Sharai, 41na Azareli, na Shelemia, na Shemaria, 42na Shalumu, na Amaria, na Yusufu. 43#Hes 32:38; Ezr 2:29Na wa wana wa Nebo; Yeieli, na Matithia, na Zabadi, na Zebina, na Ido, na Yoeli, na Benaya. 44#Mwa 6:2-5; Kut 23:2; Kum 7:3Hao wote walikuwa wameoa wanawake wageni; na wake zao wengine walikuwa wamezaa watoto.

Currently Selected:

Ezr 10: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in