YouVersion Logo
Search Icon

Wagalatia 4:8-16

Wagalatia 4:8-16 BHN

Zamani hamkumjua Mungu na hivyo mliitumikia miungu isiyo miungu kweli. Lakini sasa, kwa vile mnamjua Mungu, au tuseme mnajulikana na Mungu, mnawezaje tena kurudi kwa wale pepo maskini na dhaifu hata kutaka kuwatumikia tena? Bado mnaadhimisha siku, miezi na miaka! Nahofu kwamba labda kazi niliyoifanya kwa ajili yenu imepotea bure! Ndugu, nawasihi muwe kama mimi, kwa vile hata mimi nimekuwa kama nyinyi. Hamkunitendea ubaya wowote. Mnajua kwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia fursa ya kuwahubirieni Injili kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, wakati ule hamkunidharau wala kunikataa kwa sababu ya udhaifu wangu ingawa mlishawishiwa kufanya hivyo; lakini mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama vile ningekuwa Kristo Yesu mwenyewe. Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini? Naapa kwamba wakati ule mngaliweza hata kuyangoa macho yenu na kunipa mimi. Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu ya kuwaambieni ukweli?