Ayubu 24:22-24
Ayubu 24:22-24 NEN
Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake; ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha. Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, lakini macho yake yanaona njia zao. Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka; hushushwa na kukusanywa kama wengine wote, hukatwa kama masuke ya nafaka.