Kisha Yakobo akafanya kiapo akisema: “Ikiwa, ee Mungu, utakuwa pamoja nami na kunilinda katika safari yangu, ukinipa chakula na nguo kusudi nirudi katika nyumba ya baba yangu salama, basi, wewe Yawe utakuwa ndiwe Mungu wangu. Nalo jiwe hili nililosimika hapa kama nguzo, litakuwa nyumba yako Mungu, nami nitakupa sehemu ya kumi ya vitu vyote utakavyonipa.”