1
Wagalatia 6:9
Swahili Revised Union Version
Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
Compare
Explore Wagalatia 6:9
2
Wagalatia 6:10
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Explore Wagalatia 6:10
3
Wagalatia 6:2
Mchukuliane mizigo na hivyo kuitimiza sheria ya Kristo.
Explore Wagalatia 6:2
4
Wagalatia 6:7
Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
Explore Wagalatia 6:7
5
Wagalatia 6:8
Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Explore Wagalatia 6:8
6
Wagalatia 6:1
Ndugu zangu, mtu akishikwa katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Explore Wagalatia 6:1
7
Wagalatia 6:3-5
Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
Explore Wagalatia 6:3-5
Home
Bible
Plans
Videos