1
Mathayo 19:26
Swahili Revised Union Version
Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
Compare
Explore Mathayo 19:26
2
Mathayo 19:6
Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Explore Mathayo 19:6
3
Mathayo 19:4-5
Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamume na mwanamke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
Explore Mathayo 19:4-5
4
Mathayo 19:14
Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.
Explore Mathayo 19:14
5
Mathayo 19:30
Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
Explore Mathayo 19:30
6
Mathayo 19:29
Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
Explore Mathayo 19:29
7
Mathayo 19:21
Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Explore Mathayo 19:21
8
Mathayo 19:17
Akamwambia, Kwa nini uniulize kuhusu wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
Explore Mathayo 19:17
9
Mathayo 19:24
Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Explore Mathayo 19:24
10
Mathayo 19:9
Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
Explore Mathayo 19:9
11
Mathayo 19:23
Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Explore Mathayo 19:23
Home
Bible
Plans
Videos