“Mwana humheshimu baba yake, naye mtumishi humheshimu bwana wake. Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili? Kama mimi ni bwana, iko wapi heshima ninayostahili?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Ni ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau Jina langu.
“Lakini mnauliza, ‘Tumelidharau Jina lako kwa namna gani?’