1
Luka 6:38
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.”
Compare
Explore Luka 6:38
2
Luka 6:45
Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo maovu kutoka hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake.
Explore Luka 6:45
3
Luka 6:35
Lakini wapendeni adui zenu, watendeeni mema, wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo thawabu yenu itakapokuwa kubwa, nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu Sana, kwa sababu yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na kwa wale waovu.
Explore Luka 6:35
4
Luka 6:36
Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
Explore Luka 6:36
5
Luka 6:37
“Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa. Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa. Sameheni, nanyi mtasamehewa.
Explore Luka 6:37
6
Luka 6:27-28
“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.
Explore Luka 6:27-28
7
Luka 6:31
Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.
Explore Luka 6:31
8
Luka 6:29-30
Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyang’anya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia. Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie.
Explore Luka 6:29-30
9
Luka 6:43
“Hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri.
Explore Luka 6:43
10
Luka 6:44
Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba, wala zabibu kwenye michongoma.
Explore Luka 6:44
Home
Bible
Plans
Videos