1
Isaya 60:1
Neno: Bibilia Takatifu
“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa BWANA umezuka juu yako.
Compare
Explore Isaya 60:1
2
Isaya 60:3
Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.
Explore Isaya 60:3
3
Isaya 60:2
Tazama, giza litaifunika dunia na giza kuu litayafunika mataifa, lakini BWANA atazuka juu yako na utukufu wake utaonekana juu yako.
Explore Isaya 60:2
4
Isaya 60:22
Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu, mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu. Mimi ndimi BWANA; katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”
Explore Isaya 60:22
5
Isaya 60:19
Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, kwa maana BWANA atakuwa nuru yako ya milele, naye Mungu wako atakuwa utukufu wako.
Explore Isaya 60:19
6
Isaya 60:20
Jua lako halitazama tena, nao mwezi wako hautafifia tena; BWANA atakuwa nuru yako milele, nazo siku zako za huzuni zitakoma.
Explore Isaya 60:20
7
Isaya 60:5
Ndipo utatazama na kutiwa nuru, moyo wako utasisimka na kujaa furaha, mali zilizo baharini zitaletwa kwako, utajiri wa mataifa utakujilia.
Explore Isaya 60:5
8
Isaya 60:4
“Inua macho yako na utazame pande zote: Wote wanakusanyika na kukujia, wana wako wanakuja toka mbali, nao binti zako wanabebwa mikononi.
Explore Isaya 60:4
9
Isaya 60:21
Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu, nao wataimiliki nchi milele. Wao ni chipukizi nililolipanda, kazi ya mikono yangu, ili kuonyesha utukufu wangu.
Explore Isaya 60:21
10
Isaya 60:18
Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako, wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako, lakini utaita kuta zako Wokovu, na malango yako Sifa.
Explore Isaya 60:18
11
Isaya 60:11
Malango yako yatakuwa wazi siku zote, kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku, ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa: wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi.
Explore Isaya 60:11
12
Isaya 60:6
Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako, ngamia vijana wa Midiani na Efa. Nao wote watokao Sheba watakuja, wakichukua dhahabu na uvumba na kutangaza sifa za BWANA.
Explore Isaya 60:6
13
Isaya 60:10
“Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonyesha huruma.
Explore Isaya 60:10
14
Isaya 60:15
“Ingawa umeachwa na kuchukiwa, bila yeyote anayesafiri ndani yako, nitakufanya kuwa fahari ya milele, na furaha ya vizazi vyote.
Explore Isaya 60:15
15
Isaya 60:16
Utanyonya maziwa ya mataifa, na kunyonyeshwa matiti ya wafalme. Ndipo utakapojua kwamba Mimi, BWANA, ni Mwokozi wako, Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.
Explore Isaya 60:16
Home
Bible
Plans
Videos